8/09/2020

Mama Dangote Kitumbo "NDII" Ndoa YajibuMiongoni mwa mambo yaliyozua minong’ono kwenye ile harusi ya kukata na shoka ya dada wa staa wa muziki Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Khan, ni mtoko wa mama yao, Sanura Kassim ‘Mama Dangote’.

Mama Dangote alitinga kwenye Ukumbi wa Lugalo Golf Club, Kawe jijini Dar, wikiendi iliyopita akiwa amevaa gauni matata lililomuonesha sawia kama kitumbo chake kipo ‘ndii’!

Minong’ono ilianza mara tu baada ya mama huyo kusimama mbele ya kamera za zulia jekundu ambapo alisikika mwandishi mmoja; “Mbona kama Mama Dangote mjamzito?”

Mara baada ya kutoka kwenye zulia hilo jekundu, Mama Dangote mwenye umri wa zaidi ya miaka 50, aliacha minong’ono mingi akidaiwa kuwa huwenda ni mama kijacho kutokana na jinsi gauni hilo lilivyomkaa na kumuonesha kama ‘ameshiba’.

Hata hivyo, baadhi ya watu walisikika wakisema huwenda ameridhika tu na matunzo ya mumewe, Uncle Shamte au ni matokeo ya kujifungia kutokana na janga la Corona.

Katika tukio hilo, familia hiyo ilikuwa ikisherehekea Esma kufunga ndoa na mfanyabiashara tajiri jijini Dar, Yahaya Msizwa.

Esma ameolewa mke wa tatu kwa jamaa huyo baada ya ndoa zake mbili kuvunjika huko nyuma akiwa amejaaliwa watoto wawili na wanaume tofauti.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

1 comment:

  1. Kama si Azam Cola, basi ni mdogo wa Esma Khan.

    Hongera Anko Shamte. Tayarisha Jina kama si Yusuff basi ni Aysha.

    ReplyDelete

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger