Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

MAMBO 5 Yakumfanya Mwanamke Avumilie Kwenye Ndoa..!!!


Mahusiano mazuri kwa wanandoa au watu walio kwenye mahusiano ya kimapenzi ni moja ya mambo yanayochangia wahusika pia kuwa na afya njema na hata kuepuka baadhi ya matatizo kiafya.


Leo nmeona nikuletee mambo matano muhimu ambayo mwanamke hupenda atimiziwe na mume wake.

1. Kudekezwa & Kubembelezwa
Wanawake hupenda kubembelezwa pale wanapokuwa na huzuni, lakini pia wengi hupenda kuungwa mkono katika maamuzi yao au mawazo yao. Hivyo basi ili mwanaume uweze kumteka mwanamke wao ni lazima ujitahidi kuwa mkarimu na mwenye lugha nzuri za kubembeleza kwa mkeo.


2. Kusikilizwa shida

Wanawake hupenda pale wanapoeleza shida zao wasikilizwe vizuri na kutatuliwa matatizo yao. Inawezekana hayo matatizo yakatatuliwa kwa kuwezeshwa kifedha au hata ushari pia wakati mwingine.

3. Kuwa mstari wa mbele

Wanawake muda wote hupenda kuoneshwa kuwa wao ni wathamani kuliko wengine hivyo huhitaji kuwekwa mstari wa mbele katika mambo yao. Hali ambayo huwafanya wao kuhisi wanapendwa zaidi.

4. Kufurahishwa kwenye ndoa

Hakikisha wewe kama ni mwanaume basi katika sekta hii uwe umekamili kiasi cha kutosha yaani hata kama huna fedha, lakini hakikisha eneo hili unaliweza vizuri na unalifanya kwa ufanisi zaidi kila unapokutana na mkeo. Kwani uwapo dhaifu eneo hili basi ni rahisi sana kuyumbisha mahusiano yenu au ndoa yenu.

Kimsingi wewe kama mwanaume ni lazima utambue kuwa unawajibu wa kuhakikisha unamridhisha mpenzi/mke wako katika tendo hilo.

5. Nafasi ya kuzungumza

Kwa kawaida wanawake hupenda zaidi kujieleza kuhusu hisia zao au mambo yao kwa wale wanaohisi wanawapenda, hivyo mwanaume lazima uhakikishe unatenga muda wa kuzungumza na mpenzi wako na kumsikiliza kuhusu mambo yake na kuyafanyia kazi pale yanapoonekana yanawezekana.

Kimsingi mambo hayo yote au machache kati ya hayo yakitokea yakakosekana ndani ya ndoa kwa mda wa kipindi fulani huweza kupelekea mwanamke kuondoka na ndoa kuvunjika hivyo ni muhimu kwa wanaume kuyazingatia hayo.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments