Mamlaka Hali ya Hewa Yafafanua Tetemeko, Dar

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa kuhusu hali ya bahari kufuatia tetemeko la ardhi chini ya Bahari ya Hindi lililotokea Agosti 12, majira ya saa mbili (2) usiku, na kusema kuwa hakuna uwezekano wa kutokea Tsunami.



TMA imesema hayo baada ya kupokea taarifa zilizothibitishwa na ‘Geological Survey of Tanzania’ (GST) kuhusu tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha richteer  5.9 katika eneo la kusini mashariki mwa Mkoa wa Pwani katika Bahari ya Hindi.



Mamlaka hiyo imesema imefanya uchambuzi wa taarifa za tetemeko hilo katika kituo chake cha Tahadhari ya Tsunami na matokeo ya uchambuzi huo yanaonyesha kuwa hakuna tishio la Tsunami kutokana na tetemeko hilo. Tetemeko hilo halikuwa na nguvu kubwa na hakuna maporomoko ya ardhi yaliyojitokeza baharini ambayo yangeweza kuzalisha tsunami.



TMA inawashauri watumiaji wa eneo la bahari ikiwa ni pamoja wananchi wanaoishi katika maeneo yaliyo karibu na Bahari ya Hindi kutokuwa na hofu na kuendelea na shughuli kwa kuzingatia taarifa ya hali ya hewa baharini kama ilivyotolewa awali na mamlaka hiyo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad