8/08/2020

Man City yaitupa nje Real Madrid,Juve nayo yakwama


Klabu ya Manchester City imefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya baada ya kuifunga Real Madrid kwa bao 2-1 kwenye mchezo wa marudiano uliopigwa kwenye uwanja wa Etihad Jijini Manchester nchini Uingereza.

Manchester City ilimalizia kazi ambayo iliianza Mwezi Februari Mwaka huu ambapo katika mechi ya mkondo wa kwanza huko Santiago Bernabeu, walishinda bao 2-1 na hivyo wanafanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya bao 4-1.

Mshambuliaji Raheem Sterling ndiye aliyeitanguliza City kwa bao la uongozi dakika ya tisa kabla ya Karim Bemzema kusawazisha kwa upande wa Real dakika ya 28 kipindi cha kwanza.

Katika Kipindi cha pili Gabriel Jesus alifunga bao la ushindi dakika ya 68 lililoihakikishia ushindi Manchester City ambayo sasa itacheza dhidi ya Lyon ya Ufaransa ambayo nayo jana ikiwa ugenini ilisonga mbele licha ya kufungwa na Juventus kwa bao 2 kwa 1 lakini walifaidika kwa bao la ugenini kwani katika mechi ya kwanza walishinda bao 1-0.

Memphis Depay aliitanguliza Lyon kwa mkwaju wa penati dakika ya 12 ya mchezo lakini Cristiano Ronaldo alisawazisha kwa penati dakika ya 43 kabla ya kufunga la pili dakika ya 60 ya mchezo.

KIPI KILIGHARIMU REAL MADRID?

Kukosekana kwa nahodha Sergio Ramos kulisababisha kukosekana kwa utulivu katika idara ya ulinzi ya Real Madrid ambayo ilishuhudiwa Raphael Varane akifanya makosa makubwa matatu ambapo moja lilizaa bao,hii ilitokana na kukosekana beki kiongozi mwenye kufukia makosa,Eder Militao alikua na mlima mrefu wa kumsaidia Varane.

NDIO MWISHO WA RONALDO ULAYA?

Akiwa na umri wa miaka 35, Cristiano Ronaldo ameendelea kuwa mwiba katika michuano hii ya Ulaya,mabao yake mawili yalimfanya afikishe jumla ya mabao 130,lakini lilikua ni bao la 67 katika michezo 89 ya mtoano ya michuano hiyo.

Ronaldo ni kama Zlatan Ibrahimovic ambaye yupo na AC Milan na umri wa miaka 38 na ameendelea kufanya kazi yake ya kufunga.

Sidhani kama ndio mwisho wake,lakini kwenye ngazi ya kutwaa taji la Ulaya akiwa na Juventus ikawa ngumu kutokana na aina ya wachezaji waliopo kikosini.

Juventus ambayo inalisaka taji la Ulaya tangu mwaka 1996, imekua ikijaribu kila msimu kufikia malengo, lakini ukifuatilia katika kikosi cha jana, kocha Maurizio Sarri alikua na wachezaji takribani sita ambao wana umri wa zaidi ya miaka 30, jambo ambalo kiufundi liliwaathiri kwenye suala la kwenda na kasi ya mchezo.

VIPI LEO?

Huko Allianzi Arena majira ya saa 4 usiku , Bayern Munich itakua ikimalizia kazi waliyoianza huko Stanford Bridge ambapo walishinda kwa bao 3-0 dhidi ya Chelsea,wakati Barcelona itakua nyumbani kwao Hipsania kukabiliana na Napoli kutoka Italia na ikumbukwe katika mechi ya mkondo wa kwanza walitoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger