8/10/2020

Manara Afunguka Kuhusu Mkataba wa Chama na Tetesi za Kuhamia YangaKlabu ya soka ya Simba imesisitiza kuwa kiungo wao Clatous Chota Chama bado ana mkataba na mabingwa hao wa nchi hadi Julai 20/21.


Uthibitisho huo umetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo Haji Manara amesema nyota huyo alirefusha kwa Mwaka mmoja Mkataba huo pamoja na wachezaji wengine akiwemo mshambuliaji wao kinara , Meddie Kagere.

Manara amesema wao wataamua kumuongezea Mkataba mwingine nyota huyo na vile vile Timu yoyote na sio Yanga tu, itakayomuhitaji Kiungo huyo basi itawabidi kuwasilisha barua yenye ofa watakayoihitaji.

Katika hatua nyingine Manara amesema anashangazwa na baadhi ya wana Simba kuwa na wasiwasi na pia kuogopa maneno ya watani wao Yanga ambao kwa sasa wanadai kuwa wanaweza kumsajili mwamba huyo wa Lusaka.

Ameongeza kuwa ni ngumu kwa Klabu ya Yanga kuvunja Mkataba wa Chama kama ambavyo ilivyo ngumu kwa Simba kumsajili Feisal Salum kutoka Yanga.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger