8/21/2020

Manara: ”Wasanii Wakubwa Wanaomba Kuwepo Simba Day Kesho” -VideoOFISA Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara leo Agosti 21, 2020 amefika katika mjengo wa Global Group uliopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam kufafanya mahojiano na +255 Global Radio kuelekea kilele cha Simba Day kesho Agosti 22, 2020 Uwanja wa Mkapa.


MHARIRI Mtendaji wa gazeti la Championi, Saleh Ally (kushoto) akiwa kwenye mahojiano na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ndani ya +255 Global Radio, leo Agosti 21.

Akifanya mahojiano hayo Manara amesema kesho Simba ina ratiba nzuri ya Simba Day na kutakuwa na mechi za utangulizi,

Manara ameongeza kuwa baada ya kutangaza orodha ya wasanii watakaotumbuiza kesho wameanza  kupokea simu nyingi na maombi mengi ya wasanii wakiomba kutumbuiza kwenye tamasha hilo.

“Tumepokea simu nyingi kutoka kwa wasanii wengi tena wakubwa wakiomba kujiunga nasi kwenye tamasha letu ili waweze kuonyesha uwezo wao, ipo sawa na wana haki kwa kuwa Simba ni timu kubwa na wengi wanaipenda, kwa sasa bado tunafikiria.

Kuhusu kinachowabeba Simba ndani ya uongozi Manara amesema:-“Siri moja ya uongozi wa Simba ni usiri wa ufanyaji kazi, jambo likitokea, kesho kutakuwa na sapraizi moja kubwa, kuna mtu mmoja anadai tutamtoa Kagere kwa mkopo kisha tumtangaze mwingine.”
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger