8/21/2020

Masele Aaga Rasmi Bunge la AfrikaMakamu wa Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika, Mhe. Stephen Julius Masele ameaga rasmi Bunge la Afrika (Pan- African Parliament – PAP) baada ya muda wake kutumikia Bunge la Afrika kufikia kikomo.

Katika ujumbe wake wa kuaga Wabunge,wafanyakazi na wadau mbalimbali wa Bunge la Afrika,Masele ambaye amekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (2010-2020) amesema Mhula wa Bunge la Afrika na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vinaenda sanjari hivyo nafasi yake imefikia tamati baada ya muda wake wa Ubunge nchini kufikia tamati.

“Mhula wa Bunge la Afrika unaenda samba na mhula wa Bunge la Tanzania.Baada ya kipindi cha ubunge kuisha ambacho kinaenda na uhai wa bunge la Afrika.Nafasi yangu ya Ubunge wa Afrika pia imefikia Tamati.

Kukosa nafasi ya kugombea Ubunge kunahitimisha rasmi nafasi yangu katika Bunge la Afrika,” amesema Masele.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger