8/21/2020

Masele baada ya kutoswa Ubunge “Nimepokea kwa heshima kubwa maamuzi ya chama changu"Kikao Cha Halmashauri Kuu Kuu Ya CCM Taifa (NEC) kimetangaza Majina ya Wagombea Ubunge kwenye Majimbo watakaopeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi Mkuu 2020.

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele ambaye aliongoza katika uchaguzi wa kura maoni CCM kwa kura 152  amesema amepokea kwa heshima maamuzi ya chama chake kumtangaza Patrobas Katambi aliyeshika nafasi ya 7 kwa kura 12 katika kura za maoni kuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini katika uchaguzi mkuu 2020.
“Nimepokea kwa heshima kubwa maamuzi ya chama changu, nawashukuru wananchi wa jimbo la Shinyanga Mjini, viongozi wote wa chama changu ngazi zote kwa kunipa fursa ya kuwa mbunge kwa miaka kumi, tushikamane kukipigania chama kiweze kushinda uchaguzi mkuu, binafsi nitashiriki kikamilifu” Stephen Masele


OPEN IN BROWSER

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger