Meli Iliyobeba Ammonium Nitrate Ilifikaje Beirut?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



SERIKALI ya Lebanon imesema kuwa mlipuko mkubwa ulioharibu  maeneo kadhaa ya mji wa Beirut umesababishwa na tani 2,750 za kemikali ya ammonium nitrate iliyokuwa kwenye bandari ya mji huo.

Watu wameonyesha ghadhabu zao na kutoamini kuwa kiasi hicho kikubwa cha kemikali hatari kiliwekwa kwenye ghala bila kuzingatia hatua zozote za usalama kwa zaidi ya miaka sita, kwenye eneo hilo ambalo liko karibu sana na eneo la katikati ya mji.


Serikali haijaeleza kemikali hiyo ilipotoka, lakini kiasi hichohicho cha kemikali kiliwasili Beirut mwezi Novemba mwaka 2013 katika meli ya mizigo ya iliyokuwa na bendera ya Moldova, MV Rhosus.

Chombo hicho kinachomilikiwa na Urusi kilianza safari mwezi Septemba kutoka Batumi, Georgia, kwenda Beira, Msumbiji.

Ilikuwa imebeba tani 2,750 za ammonium nitrate, ambayo huwa katika muundo wa madonge madogo-madogo ambayo hutumika kutengenezea mbolea lakini pia inaweza kuchanganywa na mafuta kutengeneza vilipuzi kwa ajili ya shughuli za uchimbaji madini na katika sekta ya ujenzi

Wakati ikisafiri kupitia mashariki mwa Mediterranea, MV Rhosus ilipata ”tatizo la kiufundi” na ikalazimika kutia nanga bandari ya Beirut, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2015 iliyoandikwa na mwanasheria wa Lebanon aliyewawakilisha wafanyakazi wa meli hiyo.

Meli hiyo ilifanyiwa uchunguzi na maafisa wa bandari na ”kuzuiwa kufanya safari”, mawakili walisema. Sehemu kubwa ya wafanyakazi wake walirudishwa makwao, isipokuwa nahodha wa meli Mrusi, Boris Prokoshev, na wengine watatu walioripotiwa kuwa raia wa Ukraine.

Prokoshev aliliambia shirika la habari la Reuters siku ya Alhamisi kuwa meli hiyo ilikuwa inavuja, na kuwa ilipelekwa Beirut na mmiliki wake kwa ajili ya kubeba mzigo mwingine zaidi kwa sababu ya changamoto za kifedha.

Hata hivyo, wafanyakazi wa meli hiyo hawakuweza kubeba mzigo huo, na mmiliki aliposhindwa kulipa ada ya bandarini, mamlaka ya Lebanon iliizuia meli hiyo, alisema.

Muda mfupi baadaye, MV Rhosus  “ilitelekezwa na wamiliki wake kuonyesha wasiwasi kuwa hawahitaji tena mzigo,”  kulingana na wanasheria

Wakati huo huo, bado wafanyakazi walikuwa wamezuiwa kwenye chombo hicho walikuwa wakikosa chakula na mahitaji mengine. Mawakili hao walisema waliomba kwa Jaji wa Masuala ya dharura huko Beirut atoe amri ya kuwaruhusu warudi nyumbani, wakisisitiza “hatari ambayo wafanyakazi walikuwa wakikabiliana nayo kwa kuzingatia” hatari “ya shehena ya mizigo” kwenye meli.

Hatimaye Jaji alikubali kuruhusu wafanyakazi wa meli hiyo kushuka na mwaka 2014 mamlaka ya bandari ilihamisha kemikali ya ammonium nitrate na kuiweka katika ”ghala namba 12”, karibu na ghala la nafaka.

Mawakili walisema mzigo huo ulikuwa ”ukisubiri kupigwa mnada au kuharibiwa”.

”Mzigo huo ulikuwa wenye uwezo wa kulipuka. Ndio maana ulibaki ndani ya meli tulipokuwa huko…,” alisema bwana Prokoshev

Aliongeza: ”Nina masikitiko kwa watu (waliopoteza maisha au kujeruhiwa na mlipuko). Lakini mamlaka nchini humo zinapaswa kuadhibiwa. Hawakuujali mzigo huo kabisa.”

Mkurugenzi Mtendaji wa bandari, Hassan Koraytem, na Mkurugenzi wa mamlaka za mapato, Badri Daher, kwa pamoja walisema siku ya Jumatano kuwa wao na maafisa wengine walikuwa wakitahadharisha mahakama kuhusu hatari ya kuhifadhi kemikali ya ammonium nitrate na uhitaji wa kuiondoa.

Nyaraka zilizosambaa mtandaoni zilionesha barua za maafisa hao kwenda kwa jaji wa masuala ya dharura mjini Beirut wakitaka muongozo jinsi ya kuuza au kuharibu ombi ambalo lilipelekwa karibu mara sita tangu mwaka 2014 mpaka mwaka 2017.

Bwana Koraytem alikiambia chombo cha habari cha nchini humo OTV kuwa idara ya usalama pia ilituma barua za tahadhari.

Waziri wa ujenzi Michel Nijjar, ambaye ameingia madarakani mwanzoni mwa mwaka huu, aliiambia Al Jazeera kwamba alibaini uwepo wa kemikali ya ammonium nitrate mwishoni mwa mwezi Julai na kuwa alizungumza na bwana Koraytem kuhusu jambo hilo siku ya Jumatatu.

Mlipuko katika bandari ya Beirut uliua watu takribani 137 na kuwajeruhi watu karibu 5,000, wengine wakiwa hawajulikani walipo. Rais Michel Aoun amesema kuwa kushindwa kushughulikia mzigo wa meli ya Rhosus ”hakukubaliki” na kuahidi ”kuwashughulikia waliohusika na katika kitendo cha kizembe cha kupuuza na kuwaadhibu vikali.”

Serikali imeamuru maafisa waliohusika na kuhifadhi au kuongoza shughuli za kukamata mzigo wa shehena ya kemikali ya ammonium nitrate.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad