8/27/2020

Messi Atua Man CityVYOMBO vikubwa vya habari nchini Hispania vimeripoti kwamba baba mzazi wa Lionel Messi, mzee Jorge Messi, amewasili katika jiji la Manchester kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kufanya mazungumzo na Club ya Man City juu ya uhamisho wa mwanaye, Lionel Messi,  ambaye ameshaomba kuihama Barcelona.

Messi anaripotiwa kuvutiwa zaidi na Man City ili kuungana tena na kocha wake wa zamani, Pep Guardiola. Messi ameshatangaza kuwa yuko huru kuondoka Camp Nou, kitendo ambacho kimefanya mashabiki kuandamana kushinikiza  klabu hiyo isimruhusu kuondoka.

Manchester City anapewa alama 5/2 kumnunua staa huyo wa timu ya taifa ya Argentina.

Kwa mujibu wa Ripoti ya RAC1 na TyC Sports vimeeleza kuwa kuna mazungumzo ya Messi kujiunga na miamba hao wa soka kwa mkataba wa miaka miwili japo bado ni tetesi na hazijawekwa wazi na iwapo atalipwa uhamisho kwa sababu yeye ndiye ameomba kuondoka.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger