8/06/2020

Mfahamu Zaidi SarafinaMUVI ya SARAFINA ni moja ya muvi au sinema maarufu sana Afrika na dunia nzima iliyoigizwa mwaka 1992 kwa ushirikiano wa waigizaji wa Marekani (Hollywood) na wale wa Afrika Kusini iliyokuwa na lengo la kuonyesha jinsi ambavyo sera ya ubaguzi wa Makaburu dhidi ya Waafrika na wazawa wa Afrika Kusini ilivyokuwa ikiendelea na ilivyokuwa ikiwaathiri watu wa Afrika  Kusini kipindi kile ililenga zaidi mauaji ya halaiki ya wanafunzi wa Soweto nchini Afrika Kusini waliokuwa wanapinga unyanyasaji wa Makaburu hao.

Kama ulishafuatilia au kuangalia muvi hii utagundua kuwa mhusika mkuu  alikuwa Sarafina ambaye aliigiza kama mwanafunzi wa kike aliyekuwa akiwaongoza wanafunzi wenzake kupinga ubaguzi na uovu uliokuwa ukifanywa na viongozi wa Makaburu dhidi ya wananchi weusi na wazawa wa Afrika Kusini wakati ule.

Leo nimekuletea wasifu wa Leleti Khumalo maarufu kama Sarafina ili umkumbuke na kumfahamu vizuri.WASIFU WAKE

Leleti Khumalo alizaliwa 1970, ni mwigizaji wa ki-Zulu wa Afrika Kusini aliyejipatia umaarufu kutokana na nafasi yake ya kuongoza kama mhusika mkuu katika filamu ya SARAFINA!, Na katika filamu nyingine kama vile HOTEL RWANDA, YESTERDAY na INVISCUS.Leleti Khumaro alimaarufu kama Sarafina alizaliwa katika kitongoji cha KwaMashu, kaskazini mwa Durban, Afrika Kusini. Leleti Khumalo (Sarafina) alionyesha nia ya kuigiza akiwa katika umri mdogo sana, Khumalo alijiunga na kundi la vijana la kuchekesha liitwalo Amajika, lililoongozwa na Tunokwe.Mwaka 1985 alijaribu kuimba muziki akiwa na mtayarishaji na mwigizaji maarufu wa Afrika Kusini, Mbongeni Ngema, ambapo wimbo alioimba ukawa wa kimataifa ambao ulijulikana kama Sarafina!  Ngema ndiye aliyeandika sehemu kubwa ya wimbo huo wa Sarafina kwa Leleti Khumalo. Na Mbongeni Ngema ndiye mwanaume ambaye baadaye alimuoa Sarafina.Mwaka 1992, Sarafina alishirikiana sambamba na mwana mama muigizaji kutoka Marekani aitwaye Whoopi Goldberg (ambaye ndiye aliyekuwa mwalimu wa akina Sarafina katika somo la historia katika muvi ile, na alijulikana kama (Mary Masombuka), Miriam Makeba na John Kani katika filamu iliyotengenezwa chini ya kampuni ya Darell James Rootd, Filamu iliyoitwa ”SARAFINA!” ambayo ilisambazwa duniani kote, na ikawa filamu kubwa zaidi kutolewa barani Afrika. Leleti Khumalo baadaye alichaguliwa kuwania tuzo za Image pamoja na waigizaji wenzake; Angela Bassett, Whoopi Goldberg na Janet Jackson.Katika upande mwingine, mwaka 2015 Leleti alikaribishwa katika visiwa vya Zanzibar , Tanzania, kama mgeni rasmi wa sherehe maarufu za Filamu za Kiafrika ambapo waandaaji wa sherehe hiyo walikuwa wakiadhimisha miaka 18 ya sherehe hizo zinazojulikana kama Zanzibar Film Festivals.Miongoni mwa filamu ambazo mwanamama huyu aliwahi kuigiza ni;

· Uzalo (2015 -)

· Winnie Mandela (2011)

· Invictus (2009) …. Mary

· Faith’s Corner (2005) …. Faith

· Hotel Rwanda (2004) …. Fedens

· Yesterday (2004) …. Yesterday

· Cry, the Beloved Country (1995) (as Leleti Kumalo) …. Katie

· Sarafina! (1992) …. Sarafina

· Voices of Sarafina! (1988)
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger