8/31/2020

Mgombea Urais: Kuondoka kwa Messi Sio Mwisho wa DuniaMGOMBEA urais katika Klabu ya Barcelona, Toni Freixa amemjia juu staa wa timu yake, Lionel Messi kwa kusema amekosa heshima kwa klabu hiyo kutokana na kitendo chake cha kuomba kuondoka.

Toni Freixa, ni mkurugenzi wa zamani wa Barcelona anaamini kuondoka kwa Messi siyo mwisho wa dunia.

Messi ameomba kuondoka hali ambayo imemuweka kwenye matatizo rais wa sasa wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu, ambapo baadhi ya mashabiki wamekuwa wakiandamana wakimtaka rais huyo kujiuzulu.“Sipingi Messi kuondoka, kinachonishanga ni njia aliyotumia siyo ya heshima. Mkataba upo na unatakiwa kufuatwa, alipe euro 700m kisha aondoke,” alisema Freixa.

BARCELONA, Hispania
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger