Mjue Saddam Hussein wa Zaire...Kijana Katili Mtoto wa Mobutu Sese Seko Aliyekuwa Akiimbwa Kwenye Nyimbo za Wakongo..Kifo Chake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kama heading inavojieleza
Ndio zaire (DRC ya leo) aliwahi kuwepo Sadam Hussein

Kwa wale wasikilizaji wa nyimbo za zaire hasa mwishoni mwa miaka ya 90 mtakua mumewahi kusikia hili jina likitajwa sana

Saddam hussein wa zaire si mwingine bali ni kongolu mobutu.huyu ndiye alikua mfadhili mkubwa wa muziki wa zaire hasa bendi ya WENGE MUSICA BCBG Mpaka kupelekea atungiwe nyimbo na bendi hii ,wimbo huu unaitwa operation tempte du desert (operation desert storm)
Kwenye nyimbo hii vijana wa wenge musica walimsifia mno mwanzo mwisho .kwa mfano

"Kijana huyo aliyetukuka,uvaaji wake tu unaonesha tofauti"

Sio wenge musica tu waliomsifia .hadi kina koffi olomide na madilu systeme

HISTORIA YA KONGOLU
kongolu mobutu ni mtoto wa mwisho wa marechal mobutu sese seko katika ndoa ya kwanza ya rais huyo

Kongolu alikua mwanajeshi katika kikosi maalumu cha kumlinda baba yake kilichoitwa DSP(divison specialle presidentialle)

katika jeshi kongolu alikuwa na captein.

KWANINI AITWE SADDAM HUSSEIN ?

Kwa mujibu wa WIKIPEDIA kongulu kuna wakati alijihusisha na utakatishaji wa fedha halamu hivyo ikapelekea mgogoro kati yake na baba yake

Jambo lililomfanya aikimbie zaire na kwenda middle east
Rais mobutu akatuma walinzi wake waende kumrudisha kongulu nyumbani,baadae alivoamua kurudi ndio akaitwa saddam hussein

Pia kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ufaransa na marekani. Kongolu aliitwa saddam hussein kutokana na ukatili wake ,inasemwa aliogopwa sana zaire

Watafiti Wabaini Mtindo wa Mwanamke Kuwa Juu ya Mwanaume Wakati wa Tendo la Ndoa ni Hatari kwa Wanaume!


TABIA ZA KONGOLU
kama nilivosema hapo juu kuwa huyu jamaa alikua karibu sana na vijana wa wenge musica hivyo haikumaanisha muda wote vijana wa wenge hawakupata tabu sana

Inasemwa kuwa kuna siku kundi la wenge musica akiwepo werrason na wenzie walitandikwa viboko na wanajeshi waliotumwa na kongolu hadharani wakiwa kwenye shoo.kisa nini ?

Mmoja wa wanamuziki wa wenge.alitaka kuondoka zaire akajiunge na kundi la wenge la paris. Kina jb mpiana na werra son wakamnyima passport hivyo mwanamuziki huyo akaenda kushitaki kwa kongolu

Kongolu akatuma mlinzi wake mmoja akawaambie werrason na jb watoe hiyo passport,walikataa tena
Kongolu alikasirika sana kusikia hivo
Akaapa watamtambua kwani ile ni dharau
Hivyo akaamua kuwaaibisha mbele ya mashabiki


Stori ya Kutisha ya Foleni Ya Magari Iliyoganda Porini Kwa Muda Wa Miaka 70...

Haikuishia hapo. Kongulu alipata girl friend chotara ,kumbe akawa ana share demu na kijana mmoja wa wenge musica wa huko paris.
Alipokuja kujua akawafungia wenge musica kutoa album na akamwambia yule kijana wa zaire aishie paris asirudi zaire

Kongolu anatajwa kuwa ni mtu aliyependa sana anasa kwenye maisha yake ikiwemo kuchera kamari,kuendesha magari ya kifahari kwa vurugu na pia alipenda wanawake

KIFO CHA GEN MAYELE
kwa mnaofatilia au mliowahi kufuatilia matukio ya zaire mwaka 1996-1997 mtakua mliisikia hii
Mnamo mwaka 1997 waziri wa ulinzi wa zaire aliuwawa na wanajeshi wa kikosi cha rais,kwa tuhuma za usaliti
Kongolu ndie anatajwa kumuua waziri huyo,lakini kongolu wakati wa uhai wake alikataa kabisa tuhuma hizi na kudai kuwa waziri huyo alimpigia simu usiku ule na kudai kuwa yupo pale camp tshashi(haya ndio makao makuu ya ulinzi congo) ila wanajeshi hawataki kumruhusu aondoke hivyo akaomba msahada wa kongolu
Kongolu kufika akakuta waziri yuko chini kashapigwa risasi

KUIKIMBIA ZAIRE
Baada ya baba yake kuondoka zaire mnamo mwez wa 5 tarehe 15 1997 kongolu naye aliamua kuondoka
Ila kabla ya kuondoka alizunguka kila kona ya kinshasa kuwatafuta waliomsaliti baba yake.inasemekana alikua na majina ya watu zaidi ya 300 waliotakiwa kuuwawa

Baada ya kumaliza zoezi hilo kongolu anasemwa aliingia bank kuu ya zaire na kubeba dollar zote kisha kulipua na rocket runcher sehemu ya bank

Kongolu pia anatajwa kuiba mali nyingi za congo kama dhahabu almasi na copper
Ambazo aliziuza kupitia makampuni yake mengi aliyoyaanzisha

Hata hapa bongo ipo kampuni yake nimeisahau tu jina

KIFO
kongolu mobutu alikufa September 24, 1998,huko monacco akiwa na umri wa miaka 28 tu

Sababu ya kifo chake kwa mujibu wa familia ni ugonjwa wa muda mrefu

Ila kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa shirika la reuters, michella wrong anadai kongolu alikufa na UKIMWI

Watu wengi wanadai hivyo kua ukimwi ulimuua kongolu, ila kabla ya kifo cha kongolu .kaka zake walikufa pia ikasemekana kua ni uchawi wa mobutu

Hii leo watoto wa mke wa kwanza wa mobutu waliobaki ni wanawake tu.kaka zake kongulu wote wamekufa
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad