Mkwasa Kocha Mpya Ruvu Shooting

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




KLABU ya Ruvu Shooting imeachana na kocha wao Salum Mayanga na kumpa ajira kocha Boniface Mkwasa.


Afisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ameithibitishia leo Ijumaa Agosti 14, 2020 kuwa Mkwasa ni kocha mkuu mpya wa kikosi hicho.


 


Masau amesema wamemalizana vizuri na Mayanga ambaye mkataba wake ulimalizika na ameshukuru kwa utendaji kazi wake mzuri.


“Maamuzi yetu kama uongozi tumekubaliana na Mkwasa kuja kuifundisha timu yetu, kwa mkataba ambao hautaelezwa muda wake kwani ni makubaliano ya pande mbili,” amesema.


 


“Baada ya kumpata Mkwasa kama kocha wetu mkuu ndio tutaanza masuala ya usajili kwa kuangalia mapendekezo yake kwani yeye ndio atakuwa na timu,”


 


“Tunaimani chini ya Mkwasa kwa uzoefu wa soka la Tanzania aliokuwa nao tangu akiwa anacheza mpaka kufundisha tutafanya vizuri msimu ujao,” amesema Masau


 


Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Mkwasa kuifundisha Ruvu Shooting kwani aliwahi kuifundisha miaka ya nyuma na kuachana nayo alipokwenda kuwa msaidizi wa Hans Pluijm alipokuwa Yanga.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad