8/11/2020

Mlipuko Beirut: Waziri Mkuu Lebanon AjiuzuluWAZIRI mkuu wa Lebanon, Hassan Diab, ametangaza kujiuzulu kufuatia mlipuko wa wiki iliyopita mjini Beirut. Kwenye taarifa yake fupi kupitia televisheni, Diab alisema anachukua hatua hiyo ili aungane na watu wa Lebanon na kwa pamoja wapiganie mabadiliko.

Rais Michel Aoun amekubaliana na hatua hiyo ya serikali kujiuzulu. Wiki iliyopita Diab alimlaumu mtangulizi wake kwa mlipuko huo.

Alisema wanasiasa wanatakiwa kuona aibu kwa sababu ufisadi ndiyo umesababisha janga hilo lililofichwa kwa miaka saba.


Baadhi ya mawaziri tayari walikuwa wamejiuzulu hapo kabla kufuatia maandamano makubwa ya kuipinga serikali kuibuka baada ya mlipuko huo kutokea.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger