8/08/2020

Mlipuko uenda ulisababishwa na uzembe au shambulio kutoka nje- Rais wa Lebanon


u

Rais wa Lebanon Michel Aoun amesema kuwa mlipuko uliosababisha vifo vya zaidi ya watu 150 na kufanya uharibifu mkubwa mjini Beirut huenda ulisababishwa na uzembe au shambulio kutoka nje.Kupitia hotuba aliyoitoa kwa runinga, Rais Aoun amesema inawezekana tukio hilo lilisababishwa na uzembe au shambulio la roketi.Hata hivyo, Ofisi yake imesema uchunguzi wa kubaini chanzo cha mlipuko huo unaendelea.Aoun amemtaka Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa aliyeitembelea Beirut jana Alhamisi, kuhifadhi picha za anga katika eneo la tukio ili kubaini kilichotokea na iwapo Ufaransa haitakuwa na picha hizo za anga, amesema ataziulizia kutoka sehemu nyengine.


Aoun ameahidi kufanyika kwa uchunguzi kamili juu ya tukio hilo huku tayari maafisa 20 wa bandari wakikamatwa kama sehemu ya uchunguzi huo.Benki kuu nchini humo imesema imezizuia akaunti za washukiwa saba, akiwemo wakuu wa bandari na forodha.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger