8/26/2020

Morrison: Acheni Kelele Tukutane Uwanjani
NYOTA mpya wa klabu ya Simba, Bernard Morrison amesema kuwa wapinzani wao kwa msimu ujao ikiwemo klabu ya Yanga wamekuwa wakijisifu sana kutokana na usajili ambao wameufanya mpaka sasa ila anaamini kazi itaonekana uwanjani.

Morrison aliyesajiliwa na Simba kutoka Yanga alikuwa kwenye kiwango bora kwa dakika 45 alizocheza mchezo dhidi ya Vital’O kutokea nchini Burundi, mchezo uliopigwa siku ya Jumamosi kwenye Tamasha la Simba day.

Akizungumza na Championi Jumatano, Morrison alisema katika kipindi hiki cha usajili ni kawaida kwa kila mtu kujiona bora lakini uhalisia utaonekana pale ligi itakapoanza

“Unajua kwa kawaida inapofika kipindi kama hiki cha usajili kunakuwa na kelele nyingi kwa sababu kila timu inataka kuonekana imefanya usajili mzuri.

“Lakini kwa upande wangu nadhani uhalisia utaonekana tutakapokutana uwanjani hivyo tusiwe na maneno mengi tusubiri muda huo utakapofika,” alisema Morrison.

Akiwa na Yanga kwa kipindi cha nusu msimu uliopita Morrison alihusika kwenye mabao saba akifunga mabao manne na kuasisti mengine matatu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger