8/02/2020

Mr Blue Afunguka ya Moyoni "Jina la MR Blue Silipendi Hata Rangi ya Blue Siipendi Tena"


Licha ya jina la Mr. Blue kumpa MAPOZI na TABASAMU ambalo liliwateka warembo wengi tangu mwaka 2004, pia kumuingiza PESA na kuleta MBOGA SABA mezani, rapa @mrbluebyser1988 amesema halipendi jina hilo.

Rapa huyo alikuwa akizungumza kwenye mahojiano na kipindi cha HOMA kupitia @tvetanzania jana usiku ambapo alimueleza @jonijooo kwamba jina hilo halipendi kwa sababu alipewa akiwa na umri mdogo. Jina lake la kisanii alikuwa akijiita Lil Sama.

Pia Byser alisema haipendi hata hiyo rangi ya blue na haikuwahi kuwa rangi pendwa kwake.

Wimbo wa "Mr Blue" uliorekodiwa katika studio za G Records, ulibadilisha mengi kwenye maisha ya kiusanii ya Byser hata maisha binafsi pia ambapo umaarufu uliongezeka na kitaa ilikuwa ni POMBE NA MUZIKI tu!
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger