8/03/2020

Mrisho Ngasa Awaaga Mashabiki wa YangaMRISHO Ngassa kiungo mshambuliaji wa Yanga leo amewaaga rasmi mashabiki wake kwa kusema kuwa msimu ujao hatakuwa ndani ya kikosi cha Yanga. 


Kupitia ukurasa wa Instagram,Ngassa ameandakika hivi:-"Kwanza nitoe shukrani zangu kwa wote tuliokuwa pamoja katika kipindi chote, Yanga viongozi wangu mashabiki na wachezaji wenzangu kwa kikao kilichofanywa leo sitakuwa katika kikosi cha Yanga niwatakie mafanikio yalio mema. Enjoy soccer. 


Yanga kwa sasa inafanya maboresho ya kuimarisha kikosi kwa ajili ya kuongeza nguvu kwa msimu wa 2020/21. 


Kwa msimu wa 2019/20 Ngassa alikuwa miongoni mwa wazawa ambao walikuwa wanatimiza majukumu yao na alitoa pasi ya mwisho kwenye ushindi wa bao 1-0 mbele ya Lipuli Uwanja wa Samora. 


Mchezo wake wa mwisho ilikuwa ni Julai 26 wakati wakisepa na pointi tatu zilizoipa nafasi Yanga kumaliza ikiwa nafasi ya pili na pointi 72.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger