8/24/2020

Mshauri Mkuu wa Trump kuondoka IkuluMshauri wa White House Kellyanne Conway ametangaza kwamba, ataondoka katika usimamizi wa Rais wa Marekanu Donald Trump mwishoni mwa mwezi Agosti,  ambapo ameonesha nia ya kukaa na kujali familia yake.


Conway amesema kuwa anaacha kufanya kazi chini ya usimamizi wa Rais Trump na kujikita katika mahitaji ya familia yake.


"Nitakuwa nikibadilisha majukumu yangu kutoka Ikulu ya Marekani mwishoni mwa mwezi huu" amesema Conway katika taarifa yake.


Kuondoka kwake, takriban miezi miwili kabla ya Rais Trump ajaomba ridhaa ya kuchaguliwa tena kumekuja katika kipindi muhimu, ambacho kitamuacha Rais Trump bila uwepo wa mmoja wa wasemaji wake muhimu katika siasa na sera zake.


Conway alikuwa mwanamke wa kwanza na meneja wa tatu wa kampeni za Rais Trump mnamo 2016  na amekuwa mmoja wa watetezi wake waaminifu katika umma na mitandao ya habari.


Hivi karibuni alikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Rais Trump anaanzisha utaratibu wakutoa taarifa fupi mara kwa mara kuhusiana na janga la Corona katika Ikulu ya Marekani.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger