8/06/2020

Msumbiji yatangaza hali ya dharura kwa mara ya pili


Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi ametangaza siku nyingine 30 za dharuraImage caption: Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi ametangaza siku nyingine 30 za dharura
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi ametangaza siku nyingine 30 za dharura kujaribu kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

Hii ni mara ya pili kwa taifa hilo kutangaza dharura ya hali ya afya tangu mwezi Machi wakati walipothibitisha mtu wa kwanza mwenye virusi vya corona nchini humo.

Rais Nyusi alihutubia taifa kupitia matangazo ya televisheni na kuainisha hatua ambazo zitasaidia kupambana na virusi hivyo kwa urahisi .

Awamu ya kwanza kuanzia Agosti 18, taasisi za elimu ya juu zitafunguliwa , mafunzo ya jeshi na ufundi. Mikusanyiko ya dini itaruhusiwa kwa watu wasiozidi 50 . Idadi ya watu 20 mpaka 50 wataruhusiwa kuhudhuria katika msiba au mazishi lakini kwa mtu yeyote aliyekufa kutokana na virusi vya corona watu watakaomzika wasizidi 10.

Awamu ya pili itaanza Septemba; maeneo ya burudani kama sinema, ‘casino’ na sehemu za kufanyia mazoezi zitafuguliwa.

Awamu ya tatu itaanza Oktoba, wanafunzi wa sekondari ambao wako mwaka wa mwisho wa masomo watarejea shuleni.

Vilabu vya pombe vitabaki kuwa vimefungwa. Msumbiji imethibitika kuwa na maambukizi 2,079 na vifo 15.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger