8/23/2020

Mtibwa Sugar yasajili wapya watatuKlabu ya Mtibwa Sugar yenye maskani yake Morogoro huku ikitumia Uwanja wa Gairo kwa mechi za nyumbani  ambazo hazina idadi kubwa ya mashabiki huku zile za Yanga na Simba zikipigwa Uwanja wa Jamhuri umekamilisha usajili wa wachezaji watatu. 

Nyota wa kwanza kumalizana na Mtibwa Sugar alikuwa ni kiungo Abal Kassim Hamis ambaye amejiunga na klabu hiyo kwa mkopo akitokea Klabu ya Azam FC. 


Wa pili alikuwa ni George Makang’a kutoka Namungo naye ni kiungo. 


Mchezaji wa tatu ni Baraka Majogoro rasta aliyekuwa anakipiga ndani ya Polisi Tanzania naye pia ni kiungo. 


Majogoro amesema kuwa anaamini msimu ujao utakuwa na ushindani mkubwa nao watapambana kufikia malengo ya timu.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger