8/07/2020

Mungu ni Mwema! Mwili wa Mwanamke Aliyeanguka Thompson Falls WapatikanaMwili wa  Jemimah Oresha aliyetumbukia Thompson Falls, Nyahururu akipiga picha wiki mbili zilizopita hatimaye uliopolewa na wanakijiji Jumatano Agosti 5 jioni.

Naibu kamishna wa eneo bunge la Nyahururu Patrick Muli alisema mwili wa Jemima Oresha ulipatikana kilomita chache mbali na eneo alikotumbukia.


Kikosi kilichowashirikisha maafisa wa KWS, polisi, kitengo cha dharura na vile vile maafisa wa Msalaba Mwekundu kilipiga kambi katika mto huo kuusaka mwili wa marehemu.

Mwanawe mwanamke aliyeanguka Thompson falls azungumza
“Mwili huo ulionekana na wakazi wa eneo la Rwathia kando ya mto. Wakazi hao waliwajulisha polisi ambao walifika na kuuchukua.” Alizungumza Muli.

Jemimah 39, alianguka kutoka kwa jiwe alilokuwa amesimama ndugu yake akimpiga picha huku asijue kuwa atakumbana na mauti yake.

Naibu kamishna huyo aliwatahadharisha wakazi na kuwaomba kuwa waangalifu wakati wanavuka mito iliyofurika eneo hilo.

Tazama picha za mwanamke aliyeanguka Thompson Falls akichukua picha
Mwendazake alikuwa amesafiri kutoka Kitale na kwenda kutembelea jamaa zake Nyahururu ambapo alipatana na mauti yake.

Mwili wake ulipelekwa katika makafani ya hospitali ya rufaa ya Nyahururu. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger