Muuguzi Aliyepatikana na COVID19 na Kujifungua Akiwa ICU Asema Hakuwa Mjamzito

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mtoto huyo alipelekwa kwenye kiangulio huku mamake akiendelea kupata matibabu. Picha: Hisani

Sylvia Leroy alikuwa na ujauzito wa miezi saba alipopatikana na covid19

Alipatwa na mshutuko wa moyo na kufanyiwa upasuaji kujifungua akiwa ICU

Miezi mitatu baadaye, hawezi kukumbuka ikiwa alikuwa mjamzito wala kumtambua mtoto huyo

Muuguzi mmmoja wa Amerika aliyejifungua mtoto baada ya kupatikana na virusi vya corona amewaacha wengi vinywa wazi kwa kudai kuwa hakuwahi kuwa mjamzito.

Sylvia Leroy ambaye alikuwa muuguzi wa kuzalisha wajawazito alilazwa hospitalini humo akiwa na ujauzito wa miezi sita baada ya kuanza kuugua.

Baada ya vipimo, ilibainka kuwa mama huyo mwenye umri wa miaka 35 alikuwa ameambukizwa virusi vya corona hivyo akawekwa kwenye kupumizi hali yake ilizidi kuzorota.

Baada ya kukaa kwenye kipumizi hiyo kwa wiki moja, Sylvia alitolewa kwa matumaini kuwa angeweza kupumuua kivyake.

Nurse who contracted COVID-19 while pregnant can't recognise her baby

Silvia hakumbuki ikiwa alikuwa mjamzito wala kumtambua mtoto huyo. Picha: Hisani

Hapo hali yake ilikuwa mbaya zaidi akapoteza hewa kwenye ubongo kwa zaidi ya dakika nne huku akipata mshtuko wa moyo.

Madaktari hao walifanya kila wawezalo wakamuokoa mtoto huyo kwa kumfanyia upasuaji Sylvia.

Mtoto huyo alipelekwa kwenye kiangulio huku mamake akiendelea kupata matibabu.

Aidha aliripotiwa kupata jeraha la ubongo na kuathiri uwezo wake wa kukumbuka.

Dadake muuguzi huyo ameeleza kuwa Silvia hawezi kukumbuka kabisa kama alikuwa mjamzito.

Katika kisa kingine, mwanamke aliyejifungua mtoto kwenye ICU baada ya kupatikana na covid19 Kisii Kenya alifariki siku mbili baadaye.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad