Mwakyembe asikitishwa na Morrison, Simba na Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe amesema hajafurahishwa na sakata la mchezaji Bernard Morrison na Yanga kwasababu limeleta changamoto kwa Baraza la Michezo la Taifa.

Mwakyembe amesema suala hilo limeingilia sera za michezo ya nchi na kuwapa fundisho la kuangalia upya katika hizo timu mbili za Simba na Yanga, ili waone kama  zinapoleta wachezaji ziruhusiwe kupokonyana ili soka lisije kuvurugika.

''Hebu tuangalie hasa hizi timu mbili (Simba na Yanga) zinapoleta wachezaji, je ziruhusiwe kunyang'anyana wachezaji hapa hapa, kama mchezaji anaondoka kwenye timu aondoke kwanza kisha atoke huko aombe kurudi tena huku sio hapahapa itatuletea matatizo'', amesema Dr. Mwakyembe.

Mwakyembe ameongeza kuwa kwasasa hawezi kuingilia suala hilo kwani sio la kisera na kwamba TFF na wadau wengine wa soka watalimaliza na wakishindwa wanaelewa ni jinsi gani watalileta kiserikali.

Aidha waziri huyo amesema alipokea taarifa ya kutoka kwa Rais wa CAF Ahmad Ahmad, akisema hajawahi kuona ushindani wenye hamasa kubwa katika soka kama wa timu mbili za Tanzania jambo ambalo linaleta heshima kwa nchi yetu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad