8/24/2020

Mwana FA atoa sababu mbili za kugombea UbungeMgombea Ubunge Jimbo la Muheza kupitia CCM, Hamisi Mwinjuma maarufu kama MwanaFA, amesema kuwa amesukumwa kugombea jimbo la Muheza kutokana na kero mbili kuu ambazo kwa muda mrefu zimekuwa ni tatizo sugu kwa wananchi ambazo ni changamoto ya maji na barabara.
Akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhiwa fomu, amesema kuwa barabara ya Muheza hadi Amani yenye urefu wa kilometa 35 ambayo ipo katika kiwango cha changarawe ambayo kwa kipindi cha mvua huwa haipitiki, itakuwa ni kipaumbele chake katika utekelezaji wa majukumu yake.
"Watu wote tunajua kuwa Muheza kuna tatizo la maji, kwa mara ya kwanza nilikutana na mama mmoja akinionesha kichwa chake kimenyonyoka nywele akaniambia ni kwasababu ya kubeba maji, na pili wenzetu wa Amani wanapata tabu sana kwenye kipindi cha mvua barabara haipitiki", amesema Mwana FA.


Kuhusu maslahi ya wasanii amesema "nitahakikisha ninatetea mahitaji ya wasanii kwa ujumla nikiwa bungeni, nitakuwa mmoja kati ya watunga sheria,hivyo wasanii sitawaangusha".

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger