Mwanafunzi Afariki kwa Kula Chakula Harusini, 14 Walazwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza linachunguza kifo cha mtu mmoja (mwanafunzi) na watu wengine 18 walioathirika kwa kile kinachodaiwa kula chakula chenye sumu.


 


Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, tukio hilo lilitokea Agosti 24, 2020,  majira ya saa 6:00 mchana huko kituo cha afya Mwangika, Kata ya Bangwe, ilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza. ambapo mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Mwangika. Mboni Mahano (13) alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Kituo cha Afya Mwangika baada ya kudaiwa kula chakula kinachodaiwa kuwa na sumu alipokuwa kwenye sherehe ya harusi.


 


Uchunguzi wa awali umebaini kuwa Agosti 22, 2020, kulifanyika harusi nyumbani kwa Dorica Omajigo ambapo watu walikula chakula na kingine kilibaki.


 


Taarifa imeongeza kwamba Agosti 23, 2020,  wanawake na watoto wao walirudi kusafisha vyombo ndipo wakala tena chakula kilichobaki, ambapo baada ya saa kadhaa walianza kuumwa na kukimbizwa katika Kituo cha Afya Mwangika ambapo watu wazima wanne na watoto 14 wamelazwa kwa matibabu.


 


Polisi inafuatilia chanzo cha tukio hilo kabla ya kuchukua hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayebainika kuhusika na kitendo hicho.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad