8/10/2020

Mwanamke Amtoroka Mumewe wa Miaka 10 Baada ya Kugundua Anafanya Kazi ya Kuzoa Takataka


Nairobi woman quit marriage after learning husband was garbage collector, not airport employee

David alikiri kuwa alikuwa akifanya kazi za kuzoa takataka na wa la sio mfanyikazi wa uwanja wa ndege. Picha:Hisani

Shamin alijua kuwa mkewe alikuwa anafanya kazi katika kampuni ya ndege

Alikosana na jirani aliyemkejeli kwa kuolewa na mume ambaye anafanaya kazi ya kuzoa takataka

Mumewe alilazimika kukiri kuhusu kazi alikuwa akifanya, ndiyo, alikuwa akizoa takataka

David alilazimika kumfuata mkewe hadi kwao kumuomba amrudie

Je, wajua kazi anayofanya mpenzio ama mumeo? Ndoa moja imesambaratika baada ya mwanamke kugundua kuwa kazi anayofanya mume si ile aliyoambiwa.

Shamin, mkazi wa mtaa wa Embakasi mjini Nairobi alichukua hatua ya kumtema mumewe na kukataa kabisa kumsamehe na kumrudia baada ya kugundua kuwa kazi aliyokuwa akifanya siyo ile aliyojua.

Katika kipindi kimoja cha redio maarufu kama Nisamehe, Shamin alifichua kuwa mumewe alikuwa amemficha kuhusu kazi asili aliyokuwa akifanya licha ya kuishi naye kwa zaidi ya miaka kumi.

No more payment of parking fees at the exits of JKIA – Nairobi News

Siku zote, Shamin alijua kuwa mumewe, David, alikuwa mfanyikazi katika uwanja wa ndege wa JKIA. Picha: Hisani.

Mabivu na mabichi yalibainika pale alipokosana na jiraniye ambaye alimsuta akimwambia kuwa alikuwa akijishaua na mume anayefanya kazi ya takataka.

‘’Kila siku anatoka nyumbani akiwa amevalia vizuri na huwezi kujua.  Tulikuwa tukipigania maji na wanawake wengine na mmoja akajitokeza na kuniambia ‘ huwezi kujifanya hapa special na mumeo anafanya kazi ya kuzoa takataka,’  Nilijaribu kujitetea nikijua hiyo si  ukweli lakini wengine nao wakamuunga mkono, nikaona huenda kuna ukweli hapo,’ Shamin alisema.

David aliporudi nyumbani jioni hiyo, Shamin alimsihi kumwambia ukweli.

Baada ya muda, David alikiri kuwa alikuwa akifanya kazi za kuzoa takataka na wa la sio mfanyikazi wa uwanja wa ndege.

Shamin alisisitiza kuwa hakuondoka katika ndoa hiyo kwa maana mumewe alikuwa akifanya kazi ya takataka, ila alitoka maana mumewe alikuwa mwongo.

David alifanya kila nia kumsihi amsamehe na amrudie lakini wapi!

‘’ Iwapo sikukupenda, singeomba msahama kwa kusema uongo, naomba turudiane,’’ David alisema kwa upole mwingi.

Shamin alisisitiza kuwa atahitaji muda mrefu sana kufukiri kuhusu kisa hicho maana mumewe anawza kuwa na mengi sana ambayo yamefichwa.

Visa vya watu kusema uongo ili kupata wachumba vimeongezeka, baadhi ya mahusiano hayo yakidumu na mengi yakiyumbika.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger