8/12/2020

Mwanamuziki Card B Afunguka Kilichomfanya Akae Kimya Mwaka Mzima


Baada ya kuachia "Press" mwaka 2019, Cardi B alipitia kipindi cha ukimya katika muziki wake, kitu ambacho kilitengeneza maswali kwa mashabiki zake.

Ujio wa "WAP" ngoma yake mpya akiwa na Megan Thee Stallion ndio stori kubwa kwa sasa ambapo wimbo huo unazidi kufanya vizuri kwenye chart mbali mbali za dunia.

Akipiga stori na jarida la ELLE, Cardi B amesema kimya chake kilisababishwa na kutoridhishwa na mapokezi ya wimbo wake, "Press" ambao anadai haukufanya vizuri hivyo kumlazimu kuumiza kichwa zaidi kwenye ubunifu ili kuleta kitu kizuri.
-
"Watu hawakupata video yangu yoyote kwa miezi 8, hivyo walitarajia makubwa. Sikupendezwa na namna wimbo wangu "Press" wa mwisho ulivyopokelewa, hivyo ikanifanya niwekeze kwenye ubunifu. Sitaki tu niachie wimbo na kuwataka watu wanunue kwa sababu eti mimi ni Cardi, ninatakiwa niachie mziki mzuri." alisema Cardi B akiwatolea mfano Rihanna na Bruno Mars.
16h
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger