Mzee wa Utopolo awapa onyo kali Manara na Manula

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mzee wa Utopolo awapa onyo kali Manara na Manula

Hizi ni tambo za wiki ya Wananchi wa Klabu ya Yanga ambayo inakamilishwa leo kwa kutambulisha wachezaji wapya, jezi mpya na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya nchini Burundi kuanzia 11:00 Jioni kwenye Uwanja wa Benjamin William Mkapa. 


Kamera za EATV & EA Radio Digital imempata shabiki kindakindaki wa timu hiyo Mzee wa Utopolo ambaye amefunguka matarajio ya timu yake, pia amempa onyo kipa wa Simba Aishi Manula na msemaji wa timu hiyo Haji Manara juu ya uwezo wa mchezaji wao mpya Carlinhos. 


"Historia ya mchezaji wetu Carlinhos inavyosemekana makipa wengi waliokuwa wanajaribu kufuata mipira yake wameishia Hospitali, ukijaribu kufuata mipira yake mikononi basi ujue viganja hauna, namuonya sana Aishi Manula akijaribu kufuata mipira ya huyu bwana basi ni Hospitali moja kwa moja" amesema Mzee wa Utopolo 


Akizungumzia onyo lake kwa Haji Manara Mzee wa Utopolo ameongeza kusema "Ujumbe wangu kwa Manara namuomba jumapili akae kwenye station ashuhudie wananchi tunavyofaana, pia nampa onyo maana anavyoongea abakize maneno kwa sababu Oktoba hatuchezi Simba na Yanga tunacheza timu ya babu na wajukuu" 


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad