8/21/2020

Mzee Yussuf atoa tamko la kutaka kuufikisha muziki wa taarabu kimataifa


Mkali wa miondoko ya Taarab Mzee Yussuf ametoa tamko la kutaka kuufanya muziki huo kwa ukubwa zaidi kupitia Digital Platform pia anataka kuifanya taarab kupata tuzo za nje ya nchi.


Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari Mzee Yussuf amesema wamekuja na kauli mbiu yao ambayo inasema "hatuna dogo" kwa sababu hawataki kufanya jambo lolote kwa udogo bali kwa ukubwa ili kuwafikia watu zaidi.

“Nataka niifanye Taarab kama wanavyofanya wenzetu wanavyopeleka vitu vyao kwenye ‘Digital Platfrom’ maana dunia ndiyo ipo huko sasa hivi, Pia nataka Taarab ipokee tuzo za nje ya nchii hii mpaka kila mtu aseme kweli tumeamua”

Aidha, Mzee Yussuf ameongeza kusema, “Pia nataka kubadilisha zile style tulizozizoea kwenye Taarab na kuziongezea utamu zaidi kwa sababu kama kuimba tunaweza hata tukiamshwa usiku wa manane, ila kwenye video kuna mahali tunafeli”

Ikumbukwe #MzeeYussuf kwa sasa amerejea kwenye muziki wa taarab baada ya miaka mitano kupita kutangaza kuachana na muziki huo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger