Mzee Yusuf Asimulia Walivyoanza Kula Wali

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MFALME wa muziki wa taarab nchini, Mzee Yusuf, amesema kuwa alipojiunga na Bendi ya East Africa Melody Taarab akiwa mpiga kinanda, ndiyo kipindi ambacho alianza kuwa na uhakika wa yeye na familia yake kula wali kwa kuwa alianza kulipwa Sh. 1,500.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 21, 2020, wakati wa mahojiano maalumu na kipindi cha DADAZ cha East Africa Television na kuongeza hata kielimu yeye aliishia kidato cha pili.

“East Africa Melody mimi nimeanza kula kwa kulipwa 1,500, nimeenda pale nikiwa mpiga kinanda lakini nilikuwa nabeba zile speaker za pale, kila siku tukipiga shoo nne napata hela ya kununua mchele kilo tano napeleka nyumbani, uhakika wa kula wali ndiyo nilianza kuupata kipindi hicho,” ameeleza.

Aidha, ametoa neno kwa wale wanaodhani ana njaa,

“Watu wanasema huyo ana njaa ndiyo maana amerudi kuimba, kiukweli njaa tunayo sote, kama kweli wanasema hakuna njaa na anayefanya kazi ndiyo ana njaa basi sawa wao waswali tu na walale, mimi naswali na nimejiongeza na napiga na muziki wangu, sijasoma mimi nimeishia Form Two nikaacha, hii ndiyo kazi yangu,“ ameongeza.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad