8/12/2020

Namibia yakataa fidia ya mauaji ya kimbari iliyotolewa na UjerumaniRais wa Namibia Hage Geingob amekataa kupokea fidia iliyotolewa na Ujerumani kwa ajili ya mauaji ya kimbari wakati wa ukoloni.

Jeshi la Ujerumani liliuwa mamia ya maelfu ya watu wa jamii ya Herero na jamii ya Nama kati ya mwaka 1904 na mwaka 1908, wakati wa ghasia za kupinga ukoloni.


Inadaiwa pia kuwa asilimia sabini na tano (75%) ya idadi ya watu wa Herero na nusu ya idadi watu wa Nama waliuawa.

Nchi hizo mbili zilianza majadiliano juu ya fidia ya kimbari tangu mwaka 2015 na tayari wamekuwa na mazungumzo mara nane hadi sasa.Rais Geingob alikuwa anatoa muktasari wa majadiliano hayo kati ya timu ya majadiliano ya Namibia na wawakilishi kutoka Zed Ngavirue.


"Fidia iliyotolewa sasa na serikali ya Ujerumani bado haijakubaliwa na serikali ya Namibian," taarifa kutoka kwa Rais ilieleza . Aidha hakukuwa na maelezo zaidi yaliyotolewa kufafanua uamuzi huo.

"Ujerumani imekubali kuomba radhi lakini imekataa kufikia maafikiano kati yao ya kuuguza majeraha waliyoyaacha”, taarifa hiyo iliongeza.

Ukurasa wa Twitter wa ofisi ya rais wa Namibia uliweka picha ya rais Geingob na Ngavirue .

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger