Nandy Ajivunia Maisha ya Uswazi, Akana Bifu lake na Lulu Diva

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



KATI ya wasichana 10 wanaofanya vizuri katika anga ya Muziki wa kizazi kipya alias bongofleva , huwezi kuacha kumtaja mwanadada Nandy.


Nandy ambae kwa Sasa amepata dili nyinyi na kuonekana miongoni mwa wasichana wenye maendeleo.


Nandy ambae kwa sasa ni balozi wa makampuni mengi likiwemo  kampuni ya nywele aina Darling amesema pamoja na kipato chake lakini sio mtu majivuno na kujiona super star.


Nandy akizungumza na Michuzi tv wakati wa kutambulisha bidhaa mpya ya nywele ya darling amesema anapenda maisha ya kujichanganya na watu tofauti tofauti  ili ajifunze vingi.


"Mara nyingi nimekua mtu wa kula na mashabiki kwenye sehemu mbalimbali ila huwa sio mtu wa kujionyesha Sana kiasi watu wanashindwa kujua Kama huwa ni moja ya vitu ambavo napenda,"


Hata hivyo wakati huo huo nandy aliwanunulia mashabiki zake mishikaki ya shilingi elfu 25 na kuwagaia ikiwa ni sehemu ya kuonyesha kuwa anayapenda maisha ya kula pamoja na shabiki zake 


pia nandy amekanusha kuwa na ugomvi na Lulu diva.


"Ni maneno tu wala msiyafuatishe, Mimi ni shabiki wa Luludiva na Mara nyingi nasikiliza wimbo wake wa Gugugaga,"


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad