8/08/2020

Ndege ya Shirika la Air India yaanguka uwanja wa ndege wa Calicut nchini IndiaNdege ya Shirika la Air India iliyokuwa na abiria karibu 200 imeanguka katika uwanja wa ndege wa Calicut .


Ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Dubai, ilianguka wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa jimbo la Kusini mwa India, Kerala.


Shughuli za uokoaji zinaendelea, huku huduma za dharura zikiwa zinaendelea uwanjani hapo.


Bado haijafahamika kama kuna madhara yoyote yaliyotokea. Picha zilizowekwa katika mitandao ya kijamii zimeonesha ndege hiyo iliwa imevunjika vipande viwili.


Tukio hilo limetokea mwendo wa saa moja kwa saa za eneo hilo kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha


Kumekuwepo na mafuriko na maporomoko ya udongo, wakati huu wa kipindi cha monsoon. 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger