NEC yaonya vyombo vya habari vinavyotangaza waliopita bila kupingwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Siku moja baada ya kukamilika kwa zoezi la uteuzi wa wagombea wa kiti cha Urais,makamu wa rais, wabunge na madiwani Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imetoa angalizo kwa vyombo vya Habari kutotangaza majina ya wagombea waliopita bila kupingwa kabla ya tume kuwatangaza kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kusababisha vurugu.



Wakati zoezi la uteuzi wa wakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa wanawania nafasi za udiwani, ubunge Urais na makamu wa Rais likikamilika NEC inatoa angalizo hilo kufuatia baadhi ya vyombo vya Habari kuwatangaza wagombea hao jambo ambalo ni kinyume na sheria ya uchaguzi.



Kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu zitafanyika hadi Oktoba 27 huku uchaguzi mkuu ukifanyika Oktoba 28 ambapo mpaka sasa majina kumi na tano tayari yamekwishapitishwa na NEC kwa ajili ya kuwania nafasi ya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad