NEC Yatupilia mbali mapingamizi ya Tundu Lissu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Na. Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imetupilia mbali mapingamizi yote yaliokuwa yamewekwa na Mgombea wa Urais wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu dhidi ya Mgombea wa urais wa CCM Dkt John Magufuli na Mgombea Urais wa CUF Ibrahim Lipumba.

Ambapo tume hiyo imesema kuwa wagombea hao wamefuata taratibu zote za sheria ya uchaguzi na hakuna kasoro yoyote walioibaini katika mapingamizi hayo.

Kauli hiyo imetolewa usiku wa leo na  Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk Wilson  Magera wakati akizungumza na vyombo vya habari katika  Ofisi za Tume zilizopo Njedengwa jijini Dodoma.

Dkt. Mahera amesema kuwa tume imetupilia mbali mapingamizi hayo baada ya kujiridhisha kwamba pingamizi hizo hazina msingi wa kisheria hivyo kufanya wagombea hao kubaki wagombea halali wa kiti cha Urais wa Uchaguzi mkuu utakaofanyika 28 Oktoba mwaka huu  .

“Kwa msingi wa uamuzi huu vyama vya siasa vinavyo shiriki uchaguzi mkuu wa kiti cha urais na makamu wa rais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu vinabaki kuwa 15”, amesema  Dkt. Mahera.

Aidha Dkt. Mahera amesema kuwa tume imepokea pingamizi kutoka kwa Mgombea Urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu dhidi ya Prof. Ibrahim Lipumba mgombea urais CUF na  Dkt. John Pombe Magufuli mgombea kwa tiketi ya CCM.

Dkt. Mahera ameeleza kuwa tume kwa kuzingatia masharti ya kanuni ya 39 ya kanuni ndogo ya tano ya uchaguzi wa rais na wabunge za mwaka 2020 baada ya kupokea pingamizi dhidi ya wagombea hao  tume imewataarifu wawekewa pingamizi mapema na wahusika kuwasilisha utetezi wao.

Pingamizi dhidi ya mgombea wa CUF ni kwamba hakurudisha fomu za uteuzi kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na kwa mujibu wa sheria.

Dkt. Mahera amesema kuwa tume baada ya kupitia sababu za pingamizi pamoja na utetezi uliotolewa imejiridhisha kuwa Prof. Ibrahim Lipumba amerejesha fomu zake kwa mujibu wa sheria, kanuni na maelekezo ya tume ya taifa ya uchaguzi.

“Hivyo tume imejiridhisha kwamba pingamizi halina msingi wa kisheria na imetupiliwa mbali na kwa maana hiyo Prof. Lipumba anaendelea kuwa Mgombea halali wa kiti cha urais kupitia tiketi ya chama cha CUF”, amesema.

Pia Dkt. Mahera ametoa ufafanuzi kuwa pingamizi dhidi ya Mgombea wa CCM , mleta pingamizi anadai kwamba mgombea urais  kupitia CCM  Dkt. John Pombe Magufuli hakuambatanisha picha kwenye fomu ya uteuzi na hakurudisha fomu ya uteuzi kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria.

“Tume baada ya kupitia sababu za pingamizi zote mbili kwa pamoja na utetezi uliotolewa imejiridhisha kuwa Dkt. John Pombe Magufuli mgombea urais kpitia CCM amerejesha fomu zake ambazo zimeambatishwa pamoja na picha kwa mujibu wa sheria kanuni na maelekezo ya tume”,amesema.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndugu zangu, Madawa mchanganyiko yakizidi mwilini huletaga madhara, sasa tuiombe tume iongeze kipengele kuwa wagombea wawe wamethibitishwa kiafya kwambawako vizuri na wanafa katika nafasi wanayo iomba. Miaka 3
    ya kuugua na Dozi zake matatizo wake ni Vyema na ni Bora kumpeleka hapo Mirembe ili aweze kusaidiwa kwa inaelekea bado ana matatizo upstair's.

    Anatia huluma mgombea, Bora angemwachia KIBEKO.Ama nakosea Wadau.?

    ReplyDelete

Top Post Ad