8/17/2020

"Nimefanya Haya si kwa Akili Zangu" - Kigwangalla


Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamis Kigwangwalla, amesema anamaliza Uwaziri wake akiwa amepigana kwa kadri ya uwezo wake, akiamini ametoa uongozi madhubuti ulioleta mafanikio makubwa katika kudumisha na kuimarisha Utalii.Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa katika kudumisha na kuimarisha sekta ya utalii nchini, hakulala wala kuzembea wakati wa changamoto na kuongeza mapambano makali dhidi ya COVID-19.

''Nafarijika leo kuona sekta ya utalii ikianza kurejea kwa kasi nzuri kiasi na zaidi nafarijika  sana kwa mafanikio makubwa kwenye sekta ya Afya ninayoyaona leo, mengi yana mchango wangu toka nimehudumu kama Naibu waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, wazee na watoto'' ameandika Kigwangalla.

''Kwa vyovyote vile si kwa akili, ujanja, elimu wala uwezo wangu bali kwa amri ya manani na mwongozo thabiti wa Rais Dkt.John Magufuli na ushirikiano mkubwa niliopata kutoka kwa Mawaziri wenzangu, wasaidizi wangu na wananchi wote'', ameongeza.

Aidha ameandika kuwa  kuanzia wiki ijayo ataanza kutoa makala ya mafanikio katika sekta ya utalii lakini pia amemshukuru Rais Magufuli kwa kuonesha imani kwake na kwamba amemzidishia ujasiri na uvumilivu wa kuvumilia changamoto na kupambana bila uoga wala kubadili nia.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger