8/22/2020

“Nimekula kiapo mbele ya Jaji” Tundu Lissu akamilisha ujazaji fomuMgombea Urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu amekamilisha hatua za mwisho za ujazaji fomu za
uteuzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Jana August 21, 2020 Tundu Lissu akiambatana na mgombea mwenza, Salum Mwalimu, wamefika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya DSM kwa ajili ya hatua ya mwisho ya kisheria ya ujazaji wa fomu zao za kugombea.

Akizungumza baada ya kukamilisha hatua hiyo, Lissu amesema wamefika katika Mahakama hiyo kula
kiapo cha ujazaji wa fomu hizo.

“Mimi ni mteule wa CHADEMA kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania, Salum anagombea Makamu wa Rais, taratibu ya sheria ya uchaguzi baada ya kutafuta wadhamini” Lissu
“Kinachofuata ule kiapo mbele ya Jaji Mkuu, ukija kula kiapo kama sehemu ya kukamilisha ujazaji fomu ya uteuzi wa kugombea kinachofuata ni safari ya Dodoma kuwasiliha fomu za uteuzi siku ya Jumanne” Lissu 
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger