8/21/2020

Onyango wa Simba ashangazwa na wanaomuita mzee


Beki mpya wa Klabu ya Simba, Joash Onyango ameshangazwa na mashabiki na wapenzi wa kandanda wanaomuita mzee wakati yeye bado kijana.

Onyango ambaye alijiunga na Simba wiki chache zilizopita akitokea Gor Mahia ya Kenya, amesema inawezekana watu wanamuita mzee kutokana na kupaka rangi nyeupe nywele na ndevu zake.

''Nafikiri wengi wananiita mzee kutokana na rangi niliyopaka kwenye nyele na ndevu zangu,lakini kwa kweli sina haja ya kufikiria wao wanachosema''

EATV ilipomuuliza kuhusu umri wake alisema''Umri ambao mnasikia unatajwa na watu utakua ndio huo huo'' alisema Onyango.

Kuhusu kuja Simba, Onyango amesema ilikua ni ndoto yake kuja kucheza na rafiki zake aliocheza nao nchini Kenya kama Meddie Kagere na Francis Kahata ambao wote walikua Gor Mahia.

Katika hatua nyingine, Onyango alisema atahitaji kuonyesha umahiri wake ili apate namba kwa kuwa Simba ina wachezaji wazuri katia idara anayoichezea ambayo ni ya ulinzi
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger