Petitman afunguka kuhusu bifu la Wema Sepetu na KajalaMeneja na mtu wa karibu wa staa Wema Sepetu, Petetman Wakuache amesema amepanga kumaliza bifu la msanii huyo na aliyekuwa rafiki yake wa zamani na msanii mwenziye wa filamu Kajala Masanja.


Petitman Wakuache amesema  tatizo la Wema Sepetu na Kajala Masanja linazungumziwa kwa sasa ila bado hajakaa kuzungumza nao ila kuna umuhimu wa kusameheana kwa sababu maisha ni mafupi pia kuna kifo."Kuhusu suala la Wema na Kajala lipo-trending kwa sasa ukizingatia kauli ya Wema Sepetu aliyoisema, kwa upande wangu huo mchakato wa kuwapatanisha unafanyika na nina mipango hiyo ya kumaliza toafuti zao, wale ni marafiki waliokuwa nusu ndugu, matatizo yanatokea kwa binadamu na tunakoseana ila mwisho wa siku tunapatana, maisha yenyewe mafupi sana kuna kifo pia" ameeleza Petitman Wakuache

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments