8/14/2020

Polisi Yabaini Haya Ofisi za Chadema ZilizoteketeaJeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema kuwa moto uliounguza Ofisi za CHADEMA, Kanda ya Kaskazini usiku wa kuamkia leo, umeteketeza baadhi ya samani za ofisi hiyo ikiwemo, Meza, Viti na mito yake viliyokuwa nje barazani huku vioo sita vya madirisha vikivunjwa.

Taarifa hiyo imetolewa leo Agosti 14, 2020, na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Salum Hamduni, wakati akizungumzia tukio hilo, ambapo mpaka sasa hivi hakuna mtu yeyote ambaye amekamatwa kuhusika na tukio hilo.

“Mpaka sasa hivi hakuna mtu yeyote ambaye amekamatwa kuhusianaka na tukio hilo na sisi Jeshi la Polisi tunaendelea na uchunguzi ili kuweza kuwabaini wote waliohusika ili hatua za kisheria dhidi yao ziweze kuchukuliwa, nitoe wito kwa wananchi kutoa ushirikiano na kutupatia taarifa sahihi ili tuweze kuwakamata wahusika”, amesema Kamanda Hamduni.

Ofisi za CHADEMA Kanda ya Kaskazini, zimechomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo, ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene, hata mlinzi wa ofisi hiyo naye hajulikani alipo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger