8/27/2020

Pompeo afanya mazungumzo na Mwanamfalme wa Bahrain


Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo leo amefanya mazungumzo na Mwanamfalme wa Bahrain Salman bin Hamad Al-Khalifa, katika siku ya tatu ya ziara yake ya Mashariki ya Kati.

Mazungumzo hayo yanalenga kuimarisha uhusiano zaidi baina ya Israel na mataifa ya kiarabu baada ya makubaliano ya kihistoria ya kufufua mahusiano ya kidiplomasia kati ya Umoja wa Falme za Kiarabu UAE na Israel.

 Pompeo amesema kupitia ukurasa wa Twitter kwamba amegusia umuhimu wa kuimarisha amani na utulivu wa kikanda wakati wa mazungumzo hayo ili kukabiliana na ushawishi wa Iran.

Marekani inayo matumaini kwamba mataifa mengine ya kiarabu yatachukua mkondo wa UAE, ingawa serikali ya mpito ya Sudan ilisema siku ya Jumanne kuwa haina mamlaka ya kuchukua uamuzi kama huo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger