8/18/2020

Prof Jay "Mikumi Stand Up, Nimechukua Rasmi Fomu ya Kugombea Ubunge"


Msanii na Mbunge aliyemaliza muda wake Prof Jay, ametaka kuongeza muda wa kuendelea kuongoza Jimbo la Mikumi baada ya kutangaza kuchukua fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Mbunge wa Jimbo la Mikumi aliyemaliza muda wake Prof Jay akichukua fomu ya kugombea tena Ubunge kwenye Jimbo hilo.

Prof Jay ametangaza hilo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo ameandika kuwa

"Mikumi stand up, nimechukua rasmi fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Mikumi kupitia chama chetu cha CHADEMA, safari ndiyo imeanza rasmi eehh Mwenyezi Mungu nisaidie" ameandika Prof Jay 

Prof Jay ameongoza Jimbo hilo la Mikumi kwa miaka mitano iliyopita ambapo kwa mara ya kwanza aligombea Jimbo hilo mwaka 2015 na akashinda.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger