8/13/2020

Queen Darleen Afichua Kwa nini Mke Mwenza Alimpa BlockMiezi kadhaa imepita tangu dada yake Diamond Queen Darleen atangaze harusi yake hadharani na hata kufunga pingu za maisha kama mke wa pili.

Darleen alisema kuwa hajawahi kukutana wala kuzungumza na mke mwenza ana kwa na bali katika mitandao ya kijamii.

 “Sajawahi kuonana naye wala kuzunguma naye nilikuwa namuona kwenye mitandao ya kijamii lakini amenipa block, alinifuata kwenye mitandao ya kijamii kisha akaacha kunifuata kisha akanipa block.”Alisema Darleen.

Pia alisema kuwa alifahamu vyema kuwa mumewe ana mke wa kwanza na ndio maana hakuweza kumkataa.

“Kutoka kitambo nilijua ana mke ata aliponipendekeza kwake ndio maana sikukataa, haikuwa ngumu kwangu kumuoa. Sasa mimi ni mke wake ndio maana huwa naweka picha zake kwenye mitandao ya kijamii

Ndio maana nina ratiba ya siku yenye nitamposti kwenye mitandao ya kijamii.”

 Alimalizia na kusema kuwa,

“Mimi ni wa kijamii sana ni lazima niposti mume wangu, lakini kwa mke wake wa kwanza ni jambo ambalo hawakuwa wanalifanya wala kuzoea hata mkiangalia katika kurasa zake za mitandao ya kijamii hamna picha zao nyingi wakiwa wawili

Lakini ukilifanya jambo hilo kama uzoefu ni ngumu kwa maana hawakuwa wamezoea katika uhusiano wao.”
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger