8/20/2020

Raia wa nchi 130 kuingia Kenya bila Karantini


Mamlaka nchini Kenya zimetoa orodha mpya ya raia wa nchi 130 ambao wataruhusiwa kuingia nchini humo bila kukaa karantini.Hata hivyo, Taifa jirani la Tanzania halimo katika orodha hiyo. Kwa nchi za Afrika Mashariki ni Rwanda na Uganda ndizo zilizomo kwenye orodha hiyo.Kenya ilifungua anga lake Agosti Mosi na Tanzania pia haikuwemo kwenye orodha ya awali. Hali hiyo ilisababisha mamlaka za Tanzania kuzuia ndege za Shirika la Ndege la Kenya kutua nchini humo.

Licha ya viongozi wa pande zote mbili kusema wanafanya mazungumzo, bado undani ama matokeo ya mazungumzo hayo havijawekwa wazi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger