Rais wa Ufilipino "Tumieni PETROL au Diesel Kuosha Barakoa Zenu"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ameendelea kusisitiza Watu watumie petrol au diesel kuosha mask zao (barakoa) ili kuua vijidudu na kisha wazitumie tena kwa lengo la kubana matumizi, wiki iliyopita aliitoa kauli hiyo lakini Msemaji wa Serikali Harry Roque akasema Rais huyo alikuwa anatania tu, ila Duterte amejitokeza tena na kusema hakuwa anatania.

“Sijatania na huu sio mzaha, niko serious, kuna Watu baada ya kauli yangu eti wananiita kichaa mara wanasema mimi mpumbavu, kama mimi mpumbavu mbona Urais nimepewa mimi na haujapewa wewe unayejiona una akili timamu!?, nimeongea ukweli kama unakosa kemikali za kuua wadudu kwenye barakoa hasa kwa masikini nenda kwenye kituo cha petrol au diesel na uisafishe barakoa yako hasa zile za vitambaa” -Rais Duterte
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad