Rasmi Sasa, Senzo Wa Simba Ni Mali Ya Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



UONGOZI wa Yanga, rasmi leo umemtambulisha Senzo Mbatha kuwa mfanyakazi wao ndani ya klabu hiyo akitokea Klabu ya Simba.


 


Senzo alijiuzulu nafasi yake ndani ya Simba hivi karibuni na kuzua mshtuko mkubwa kwa wanachama na viongozi wa klabu yake ya zamani kwa kuwa hawakujua anaweza kuibukia kwa watani zao wa jadi.


 


Akiwa ndani ya Simba, Senzo aliweza kuiongoza Simba kwa mafanikio makubwa na kusimamia usajili wa mchezaji wao nyota Luis Miqussone ambaye inaelezwa kuwa alikuwa kwenye hatua za mwisho kuibukia Yanga.




Sababu kubwa ya Senzo kusepa ndani ya Simba inaelezwa kuwa mkataba wake ulikwisha na mabosi wa Simba waligoma kumuongezea mkataba mwingine jambo lililomfanya bosi huyo abagwe manyanga kabla ya muda wake kuisha jumlajumla kwenye mkataba wake.


Leo, Agosti 20, Yanga wamemkaribisha kiongozi huyo Jangwani rasmi ndani ya klabu hiyo ambayo kwa sasa inaboresha kikosi chake.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad