8/22/2020

RC Mwanza amwagiza DC Sengerema kusimamia msibaMkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Emmanuel kipole kusimamia shughuli zote za mazishi katika msiba uliotokea  wilayani  humo  baada ya nyumba kuungua  moto iliyouwa watu sita usiku wa kuamkia ijumaa ya Agosti 21. 


Mongella ametoa agizo hilo leo Agosti 22, 2020, alipofika msibani hapo kutoa pole kwa familia na  kuwataka kujifunza kutokana na msiba huo na pia kumuombea majeruhi mmoja ambaye bado anaendelea na matibabu ili aweze kupona haraka. 


‘’Kufiwa na ndugu wa familia moja tena kwa mpigo si jambo rahisi sana, majeruhi mmoja aliyepo hospitali tunamuombea kwa mungu aweze kupona haraka, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya na timu yako msimamie hilo ili kwa upande wa serikali mtuwakilishe  na muhakikishe hayo mazishi yafanyike kwa heshima kama inavyostahili’’, amesema Mongella. 


Naye kamanda wa zimamoto mkoani Mwanza  Ambwene Mwakibete amesema uchunguzi bado unaendelea na taarifa za awali zinaonesha kuwa huenda moto huo umesababishwa na hitilafu ya umeme.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger