8/22/2020

Rich Mavoko ajibu anavyomchukulia HarmonizeMessi wa BongoFleva Rich Mavoko amefunguka kusema ilikuwa mipango na malengo yake kuwa kimya kwa muda mrefu, na comment aliyoiachia Harmonize kwenye mtandao wa Instagram kuhusu ukimya wake anaitafsiri kama ni hisia kwani aliishi naye vizuri. 


Rich Mavoko ameendelea kusema ilikuwa ni lazima kurudi nyuma na kupanga vitu sawa ndiyo maana aliamua hata asiwepo kwenye mitandao ya simu ili kuji-update na kuwa mpya. 


"Wakati Harmonize anaandika ile comment nilikuwa sina mawasiliano naye, pili niliichukulia kama alikuwa hajui nipo wapi na nafanya nini labda kwa sababu alihisi kuna vitu vinaongeleka, alikuwa na haki ya kuandika anachohisi kutokana hisia zake na aliyokuwa anayaona, pia yule ni mdogo wangu na niliishi naye vizuri" ameeleza Rich Mavoko 
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger